Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version (Neno) 2015

Hosea 3:1-5

Upatanisho Wa Hosea Na Mkewe

1Bwana akaniambia, “Nenda, ukaonyeshe upendo wako kwa mke wako tena, ingawa amependwa na mwingine naye ni mzinzi. Mpende kama Bwana apendavyo Waisraeli, ingawa wanageukia miungu mingine na kupenda mikate mitamu ya zabibu kavu iliyowekwa wakfu.”

2Basi nilimnunua huyo mwanamke kwa shekeli kumi na tano3:2 Shekeli 15 za fedha ni sawa na gramu 170. za fedha, pia kwa kiasi kama cha homeri moja na nusu3:2 Homeri moja na nusu ni kama lita 330. ya shayiri. 3Kisha nilimwambia, “Utaishi nami kwa siku nyingi, hupaswi kuwa kahaba au kuwa na uhusiano wa karibu na mtu yeyote, nami nitaishi na wewe.”

4Kwa maana Waisraeli wataishi siku nyingi bila kuwa na mfalme wala mkuu, bila kuwa na dhabihu wala mawe matakatifu, bila kisibau wala sanamu. 5Baadaye Waisraeli watarudi na kumtafuta Bwana Mungu wao na Daudi mfalme wao. Watakuja wakitetemeka kwa Bwana na kwa baraka zake katika siku za mwisho.