Biblica® Open Kiswahili Contemporary Version (Neno) 2015

Zaburi 149:1-9

Zaburi 149

Wimbo Wa Kumsifu Mungu Kwa Wema Wake

1Msifuni Bwana.

Mwimbieni Bwana wimbo mpya,

sifa zake katika kusanyiko la watakatifu.

2Israeli na washangilie katika Muumba wao,

watu wa Sayuni na wafurahi katika Mfalme wao.

3Na walisifu jina lake kwa kucheza

na wampigie muziki kwa matari na kinubi.

4Kwa maana Bwana anapendezwa na watu wake,

anawavika wanyenyekevu taji ya wokovu.

5Watakatifu washangilie katika heshima hii,

na waimbe kwa shangwe vitandani mwao.

6Sifa za Mungu na ziwe vinywani mwao

na upanga ukatao kuwili mikononi mwao,

7ili walipize mataifa kisasi

na adhabu juu ya mataifa,

8wawafunge wafalme wao kwa minyororo,

wakuu wao kwa pingu za chuma,

9ili kuwafanyia hukumu iliyoandikwa dhidi yao.

Huu ndio utukufu wa watakatifu wake wote.

Msifuni Bwana.