Zaburi 150
Msifuni Bwana Kwa Ukuu Wake
1Msifuni Bwana.
Msifuni Mungu katika patakatifu pake,
msifuni katika mbingu zake kuu.
2Msifuni kwa matendo yake makuu,
msifuni kwa kadiri ya wingi wa ukuu wake.
3Msifuni kwa mvumo wa tarumbeta,
msifuni kwa kinubi na zeze,
4msifuni kwa matari na kucheza,
msifuni kwa kinanda cha nyuzi na filimbi,
5msifuni kwa matoazi yaliayo,
msifuni kwa matoazi yavumayo sana.
6Kila chenye pumzi na kimsifu Bwana.
Msifuni Bwana!